Ufahamu kwa kina ugonjwa wa UTI | UTI Ni nini?

  • Ugonjwa wa UTI ni maambukizi yanayotokea katika sehemu yoyote ya mfumo wa mkojo (maambukizi katika njia ya mkojo). Mfumo huu unajumuisha figo, mirija ya mkojo (ureters), kibofu na urethra.
  • Maambukizi mengi hutokea katika sehemu za chini za mfumo wa mkojo — yaani kibofu na urethra.
  • Wanawake wako kwenye hatari kubwa zaidi ya kupata UTI kuliko wanaume. Ikiwa maambukizi yatabaki kwenye kibofu tu, huweza kuwa na maumivu na usumbufu. Hata hivyo, matatizo makubwa ya kiafya yanaweza kutokea ikiwa maambukizi yataenea hadi kwenye figo.
  • Watoa huduma za afya mara nyingi hutibu UTI kwa kutumia antibiotiki. Pia, unaweza kuchukua hatua mbalimbali ili kupunguza hatari ya kupata UTI.
ugonjwa wa uti

Makala zaidi: Sababu za uke kujamba | Mambo 7 Muhimu Kuyajua.

Dalili za uti Ni zipi?

UTI haziwezi kuonesha dalili za moja kwa moja kila wakati. Lakini zikijitokeza, zinaweza kujumuisha dalili hiizi zifuatazo:

  • Hisia ya kuhitaji kukojoa mara kwa mara zisizokwisha
  • Maumivu wakati wa kukojoa (Kama mkojo unaunguza)
  • Kukojoa mara kwa mara huku ukitoa mkojo kidogo sana
  • Mkojo unaoonekana na ukungu (Mawingu mawingu)
  • Mkojo wenye rangi nyekundu, waridi mkali au kama soda ya coca cola —Hii ni  ishara ya damu kwenye mkojo Kuontesha kuwa huenda maambukizi yamefika kwenye figo.
  • Kupata Mkojo wenye harufu kali
  • Maumivu ya nyonga, hasa kwa wanawake — katikati ya nyonga au karibu na mfupa wa kinena
wasiliana na doctor online

Kwa watu wazima waliozeeka, UTI huweza kufichika au kuchanganywa na hali nyingine za kiafya.

UTI sugu ni hali ambapo mtu hupata maambukizi ya njia ya mkojo mara kwa mara, kwa mfano:

  • Mara mbili au zaidi ndani ya miezi 6
  • Au mara tatu au zaidi ndani ya mwaka mmoja
dalili za ugonjwa wa uti

Makala zaidi: Madhara ya p2 Usiyoyajua Chukua Tahadhari Mapema

Dalili za UTI sugu: Baadhi ya Dalili kuu

  • Dalili za UTI sugu ni kama zile za UTI ya kawaida, lakini huwa zinajirudia mara kwa mara, au haziponi kabisa licha ya matibabu. Zinaweza kujumuisha:

Dalili za UTI sugu:

wasiliana na doctor online
  1. Kupata maumivu wakati wa kukojoa
  2. Kukojoa mara kwa mara kwa kiasi kidogo, hata mara tu baada ya kukojoa
  3. Mkojo wenye ukungu au harufu kali isiyo ya kawaida
  4. Kupata Damu kwenye mkojo – rangi ya waridi, nyekundu au ya kahawia
  5. Kupata Maumivu ya tumbo la chini (chini ya kitovu na kwenye nyonga)
  6. Kuhisi haja ya dharura ya kukojoa, hata kama kibofu hakijajaa
  7.  Maumivu ya mgongo au pembeni mwa mbavu (ikiwa figo zimeathirika)
  8. Homa au baridi (dalili ya maambukizi ya figo ikiwa yameenea juu)
  9. Kuchoka au kutojisikia vizuri kwa muda mrefu

UTI wa mgongo:

uti wa mgongo

Makala zaidi: Kutokwa na uchafu ukeni Mambo 8 Usiyoyajua.

  • UTI kwa mgongo si jina linalotumika rasmi katika tiba, lakini mara nyingi watu hutumia istilahi hiyo kumaanisha maambukizi ya njia ya mkojo ambayo yameenea hadi kwenye figo, na kusababisha maumivu ya mgongo, hasa sehemu ya juu au pembeni mwa mgongo.
  • Katika huduma hii tiba, hali hii inajulikana kama:
wasiliana na doctor online

👉 Pyelonephritis (yaani maambukizi ya figo)

Dalili za UTI iliyoenea hadi kwenye figo (pyelonephritis):

  1.  Maumivu ya mgongo au ubavuni (karibu na mbavu upande mmoja au wote)
  2. Homa kali — joto la mwili hupanda ghafla
  3. Baridi kali na kutetemeka
  4. Kichefuchefu na kutapika
  5. Kuwashwa au maumivu wakati wa kukojoa
  6. Kukojoa mara kwa mara, mkojo kidogo na wenye harufu mbaya
  7. Damu kwenye mkojo au mkojo wenye rangi isiyo ya kawaida
  8. Kuchoka kupita kiasi au hali ya kutojisikia vizuri
wasiliana na doctor online

Aina za UTI Maambukizi ya Njia ya Mkojo

Kila aina ya UTI inaweza kuleta dalili maalumu, kulingana na sehemu ya mfumo wa mkojo iliyoathirika:

Visababishi Vikuu vya Uti

dalili za uti sugu

Makala zaidi: Usiyoyajua Kuhusu Ugonjwa wa PID: Dalili 7 za pid Za Mapema.

  • UTI hutokea pale ambapo bakteria wanapoingia kwenye njia ya mkojo kupitia urethra (mrija wa mkojo) na kuanza kuenea kwenye kibofu (Fuko la mkojo). Ingawa mfumo wa mkojo umeundwa kuzuia bakteria, mara nyingine kinga hii huelemewa na kushindwa. Hali hiyo hupelekea bakteria kukua na kusababisha maambukizi hayo.
wasiliana na doctor online

UTI za kawaida hutokea zaidi kwa wanawake na huathiri kibofu na urethra:

Maambukizi Yakiwa kwenye Kibofu

  • Aina hii ya UTI mara nyingi husababishwa na bakteria waitwao Escherichia coli (E. coli),wanaopatikana kwa kawaida katika mfumo wan jia ya haja kubwa (Mkundu). Lakini mara nyingine, bakteria wengine huweza kuwa chanzo.
  • Kufanya ngono pia kunaweza kusababisha maambukizi kwenye kibofu, lakini si lazima uwe unajamiiana ili kupata maambukizi. Wanawake wote wapo katika hatari ya kupata UTI kutokana na muundo wa miili yao.
  • Urethra ya mwanamke ipo karibu na mkundu, na pia karibu na kibofu (ni fupi sana). Hali hii hurahisisha bakteria kutoka kwenye mkundu kuingia kwenye urethra na kufika hadi kwenye kibofu.

Maambukizi Yakiwa kwenye Urethra

wasiliana na doctor online
  • Maambukizi Haya hutokea pale ambapo bakteria kutoka kwenye mfumo wa chakula na husambaa hadi kwenye urethra (mrija wa mkojo). Pia, magonjwa ya zinaa kama vile herpes, kisonono, chlamydia na mycoplasma yanaweza kusababisha maambukizi ya urethra, hasa kwa sababu urethra ya wanawake ipo karibu na uke.

Vitu Vinavyoongeza Hatari ya kupata UTI

Vitu vinavyosababisha ugonjwa wa uti

Makala zaidi:Ijue Mimba ya Wiki Moja: Dalili 7 Muhimu za Awali.

UTI ni ya kawaida kwa wanawake, na wanawake wengi hupata zaidi ya mara moja katika maisha yao.

Sababu zinazoongeza hatari ya UTI kwa wanawake ni pamoja na:

  • Maumbile ya kike: Wanawake wana urethra fupi kuliko wanaume, hivyo bakteria husafiri kwa urahisi kufika kwenye kibofu.
  • Ngono: Kufanya ngono mara kwa mara huongeza hatari ya kupata UTI, na kuwa na mpenzi mpya pia huongeza hatari.
  • Njia za kupanga uzazi: Kutumia diaphragms na dawa za kuua mbegu za kiume (spermicides) huongeza hatari ya UTI.
  • Menopause: Kupungua kwa homoni ya estrogen baada ya kukoma hedhi husababisha mabadiliko kwenye njia ya mkojo yanayoweza kuongeza hatari ya UTI.
wasiliana na doctor online

Sababu nyingine ni pamoja na:

  • Matatizo ya kuzaliwa ya njia ya mkojo: Watoto wanaozaliwa na matatizo kwenye mfumo wa mkojo wanaweza kuwa na matatizo ya kutoa mkojo, hivyo mkojo hurudi nyuma na kusababisha UTI.
  • Vizuizi kwenye njia ya mkojo: Mfano kama una Mawe kwenye figo au kibofu kilichojaa kutokana na mkojo kukwama kwa mgonjwa wa tezi dume huweza kuongeza hatari ya uti.
  • Upungufu wa kinga mwilini: Magonjwa kama kisukari hupunguza kinga ya mwili na kuongeza uwezekano wa kupata UTI.
  • Matumizi yatokanayo na katheta: Watu wasioweza kukojoa wenyewe hutumia mirija ya kutoa mkojo (katheta), ambayo huongeza hatari ya UTI.
  • Upasuaji wa njia ya mkojo au vipimo vya ndani vya mfumo wa mkojo vinaweza pia kuongeza uwezekano wa maambukizi.

Madhara (Matatizo) Yanayoweza Kutokana na UTI

wasiliana na doctor online

Maambukizi ya sehemu za chini za mfumo wa mkojo mara chache husababisha matatizo ikiwa yatatibiwa mapema. Hata hivyo, yasipotibiwa, yanaweza kusababisha matatizo makubwa ya kiafya kama:

  • Maambukizi ya mara kwa mara Kujirudia— zaidi ya mara mbili kwa miezi sita au zaidi ya mara tatu kwa mwaka.
  • Kupata Uharibifu wa kudumu wa figo kutokana na maambukizi yasiyotibiwa.
  • Kujifungua mtoto njiti au mwenye uzito mdogo hupelekea UTI hutokea wakati wa ujauzito.
  • Kusinyaa kwa urethra kwa wanaume kutokana na maambukizi ya mara kwa mara.
  • Maambukizi makali kuenea mwilini (Sepsis) — hali hatari inayotokana na maambukizi kuenea mwilini, hasa ikiwa yamefika kwenye figo.

Jinsi ya kujikinga na UTI

wasiliana na doctor online

Hatua hizi zinaweza kusaidia kupunguza hatari ya kupata UTI:

  • Kunywa maji ya kutosha, hasa maji safi. Husaidia kufuta mkojo mara kwa mara na kuondoa bakteria.
  • Jaribu juisi ya cranberry. Tafiti kuhusu faida zake bado hazijathibitisha moja kwa moja, lakini ina matokeo makubwa katika kusafishanjia ya mkojo..
  • Jisafishe kutoka mbele kwenda nyuma baada ya kujisaidia haja kubwa ili kuzuia kueneza bakteria kutoka mkunduni hadi ukeni au kwenye urethra.
  • Kojoa mara baada ya tendo la ndoa. Pia kunywa glasi ya maji ili kusaidia kuosha bakteria, watoke nje kwa urahisi.
  • Epuka kutumia bidhaa zinazokera sehemu za siri, vitu kama dawa za kunyunyiza manukato, dawa za kusafisha uke, Pamoja na poda.
  • Badilisha njia ya uzazi wa mpango. Diaphragms, kondomu zisizo na vilainishi, au zenye dawa ya kuua mbegu huweza kuchangia kukua kwa bakteria wengi zaidi ambao huleta shida ya uti.
wasiliana na doctor online

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *