Madhara ya P2 (Postinor-2): na Kila Kitu Unachopaswa Kujua Kabla ya Kutumia Vidonge Hivi vya Dharura
- Katika dunia ya sasa ambapo taarifa za afya ya uzazi zinapatikana kwa urahisi, ni muhimu wanawake wajue si tu matumizi sahihi ya dawa za kupanga uzazi wa dharura, bali pia madhara ya p2 yanayoweza kujitokeza baada ya matumizi. Moja ya dawa maarufu kwa ajili ya dharura ni Postinor-2, inayojulikana pia kwa kifupi kama P2. Dawa hii hutumiwa kuzuia mimba baada ya kushiriki tendo la ndoa bila kinga au pale ambapo njia nyingine ya uzazi imeshindwa, mfano kondomu kupasuka.
- Licha ya manufaa yake, kama ilivyo kwa dawa nyingine yoyote, P2 ina madhara ambayo baadhi yake ni ya kawaida na mengine ni ya nadra lakini muhimu kujua. Katika makala hii, tutachambua kwa undani madhara haya, jinsi yanavyojitokeza, nini cha kufanya unapoyaona, na jinsi ya kujitayarisha kabla ya kuamua kutumia Postinor-2.

Makala zaidi: Sababu za uke kujamba | Mambo 7 Muhimu Kuyajua.
Madhara ya P2 ya kawaida (Zaidi ya 1% ya Watumiaji)
- Haya ni madhara ya p2 ambayo hutokea kwa zaidi ya asilimia moja ya wanawake wanaotumia P2. Hata kama madhara ya p2 haya hayatatokea kwa kila mtumiaji, ni ya kawaida na hayapaswi kukupa wasiwasi mkubwa. Kwa kawaida huisha bila matibabu maalum ndani ya siku chache baada ya matumizi.
1. Kichefuchefu na Kutapika
- Hili ndilo tatizo la kwanza ambalo wanawake wengi hulalamikia baada ya kutumia P2. Kichefuchefu huweza kuanza saa chache baada ya kumeza dawa na kwa baadhi ya wanawake huweza kuambatana na kutapika.
- 👉 Tahadhari: Ikiwa utatapika ndani ya saa 2 baada ya kumeza kidonge, huenda dawa haijafanya kazi kikamilifu. Katika hali hii, ni vyema kuwasiliana na daktari ili uandikiwe dozi nyingine ya ziada.
2. Kuharisha
- Kuharisha ni dalili nyingine ambayo baadhi ya wanawake hupata, hasa wale wenye tumbo nyeti au wanaopata msongo wa mawazo baada ya kutumia dawa. Kwa kawaida, hali hii huwa ya muda mfupi na huisha bila matibabu.
3. Kizunguzungu
- Kuna baadhi ya wanawake ambao huripoti kuhisi kama wanazunguka au kama dunia inazunguka, hali inayojulikana kama kizunguzungu. Hii hutokea kutokana na mabadiliko ya homoni au kushuka kwa shinikizo la damu baada ya kutumia P2.
4. Maumivu ya Kichwa
- Homoni ya levonorgestrel ambayo ndio kiambato kikuu cha P2, inaweza kusababisha maumivu ya kichwa kwa baadhi ya wanawake. Maumivu haya kwa kawaida huwa madogo hadi ya wastani, na huisha baada ya siku moja au mbili.
5. Maumivu ya Matiti
- Matiti kuwa laini au kuuma ni dalili nyingine ya kawaida. Hali hii inahusiana na mabadiliko ya homoni ambayo hutokea mwilini baada ya kutumia P2. Mara nyingi huisha yenyewe baada ya siku chache.
6. Kutokwa na Damu Ukeni (Spotting)
- Baadhi ya wanawake huripoti kuona matone madogo ya damu (spotting) siku chache baada ya kutumia dawa. Hii si hedhi, bali ni athari ya mabadiliko ya homoni. Wengine pia huripoti hedhi yao kuanza mapema au kuchelewa.
7. Uchovu
- Kujisikia mchovu au kuishiwa nguvu ni hali ya kawaida ambayo huambatana na matumizi ya P2. Mabadiliko ya homoni huathiri mfumo wa mwili mzima, hivyo ni jambo la kawaida kwa mwili kuhisi umekuwa mzito au umechoka.

Makala zaidi: Ijue Mimba ya Wiki Moja: Dalili 7 Muhimu za Awali.
Madhara Yasiyo ya Kawaida ya dawa za p2 (Chini ya 1%)
- Haya ni madhara ya p2 ambayo hutokea kwa wanawake wachache sana, lakini ni muhimu kuyajua kwani yanaweza kuashiria hali inayohitaji uangalizi wa haraka wa kiafya.
1. Mimba ya Nje ya Mfuko wa Uzazi (Ectopic Pregnancy)
- Hii ni hali hatari ambapo kiinitete hujipandikiza nje ya mfuko wa uzazi, mara nyingi kwenye mirija ya falopia. Ingawa ni nadra, mimba ya aina hii inaweza kuhatarisha maisha ikiwa haitagundulika mapema. Dalili zake ni pamoja na maumivu makali ya tumbo upande mmoja, kutokwa na damu isiyo ya kawaida, na kizunguzungu kikali.
- 👉 Tahadhari: Ikiwa baada ya kutumia P2 unahisi maumivu makali ya tumbo au hedhi yako haijarudi baada ya wiki tatu, fanya kipimo cha mimba au muone daktari mara moja.
2. Chunusi (Acne)
- Kwa baadhi ya wanawake, P2 huweza kusababisha mlipuko wa chunusi kutokana na athari za homoni. Ingawa hali hii si hatari, inaweza kusababisha msongo wa mawazo kwa wanawake wanaojali muonekano wa ngozi yao.
3. Dalili za Mafua
- Hii inaweza kujumuisha hali ya mwili kuwa baridi, uchovu, na homa ya mwili. Dalili hizi zinaweza kufanana na mafua ya kawaida, lakini ni athari ndogo zinazojitokeza kwa wachache baada ya kutumia dawa.

Makala zaidi: Usiyoyajua Kuhusu Ugonjwa wa PID: Dalili 7 za pid Za Mapema.
Nini Ufanye Ukiona Madhara ya p2s?
✔️ Epuka hofu isiyo ya lazima: Madhara ya p2 mengi ni ya muda na hupotea bila tiba.
✔️ Fanya kipimo cha mimba: Ikiwa hedhi yako itachelewa kwa zaidi ya wiki moja au ikawa nyepesi kupita kawaida.
✔️ Wasiliana na daktari: Ikiwa utatapika mara kwa mara, kupata maumivu makali ya tumbo au dalili nyingine zisizo za kawaida.Bofya Hapa
Hitimisho: Je, Inafaa Kutumia P2?
- P2 ni dawa salama kwa matumizi ya dharura, lakini si ya kutegemewa kama njia ya kudumu ya kupanga uzazi. Madhara ya p2 kwa ujumla ni madogo na ya muda mfupi, Kama ukitumia kidogo, lakini usipuuze dalili yoyote inayokuacha na wasiwasi. Kama utaifanya kuwa kama njia yako ya uzazi wa mpango ya mara kwa mara, basi itakuletea madhara makubwa kiafya, ikiwemo Mimba kutunga nje ya kizazi, na kupata shida ya kushika mimba baadae.