Fahamu Kila kitu Kuhusu Kutokwa na Uchafu Ukeni (Vaginal Discharge) Aina za uchafu na maana zake- Sababu zake na Matibabu.
- Kutokwa na uchafu ukeni ni Hali ya kutokwa na ute mweupe au wa rangi ya uwazi unaotoka ukeni. Hali hii ni ya kawaida, lakini mabadiliko katika kiasi, Mwonekano, rangi au harufu ya kutokwa na uchafu ukeni hiyo yanaweza kuashiria maambukizi au tatizo jingine la kiafya.

Makala zaidi: Sababu za uke kujamba | Mambo 7 Muhimu Kuyajua.
1.Je uchafu wa kawaida wa ukeni Unakuwaje?
- hali ya kutokwa na uchafu ukeni kwa kawaida inapaswa kuwa mweupe au mwepesi wenye mwangaza, usiwe na harufu mbaya, na unene wake unaweza kubadilika kulingana na mzunguko wa hedhi. Sifa nyingine za uchafu wa kawaida ni:
- Muundo wake: Ni kawaida kwa uchafu wa uke kuwa mwembamba (laini), wa kunata, mzito au wenye mnato. Homoni za mwili husababisha mabadiliko haya, lakini maambukizi pia yanaweza kuathiri umbile la uchafu. Lakini Ikitokea Uchafu unakuwa wenye chembechembe, povu au unaoambatana na kuwashwa au mabadiliko ya rangi unaweza kuwa ishara ya maambukizi Ukeni.
- Rangi ya uchafu unaotoka ukeni: Rangi ya uchafu wa kawaida huwa angavu (clear), mweupe au wenye weupe wa maziwa. Rangi ya njano iliyokolea, kijani, kahawia au kijivu inaweza kuashiria maambukizi maambukizi ukeni au kwenye kizazi.
- Harufu: Uchafu unaweza kuwa na harufu ya kawaida isiyo kali. Ikiwa unapata harufu kali kama ya samaki au harufu mbaya inayoambatana na mabadiliko ya muundo au rangi, unaweza kuwa na maambukizi ukeni au kwenye kizazi.
- Kiasi cha uchafu: Kiasi cha kutokwa na uchafu ukeni hutofautiana kati ya mtu na mtu. Wakati wa Ujauzito, kipindi cha kutumia vidonge vya uzazi wa mpango, au wakati wa ovulation (Siku za kutunga mimba) Kiwango kinaweza kuongeza kiasi. Mabadiliko ya ghafla katika kiasi cha uchafu yanaweza kuashiria tatizo fulani.
2.Wasiliana na mtoa huduma wa afya endapo utagundua Moja wapo ya mambo yafuatayo:
- Kuongezeka kwa kiasi cha kutokwa na uchafu ukeni.
- Mabadiliko ya rangi ya uchafu.
- Harufu kali au mbaya.
- Mabadiliko katika umbile au muundo wa uchafu.
- Kuwashwa, maumivu au muwasho ndani ya uke au karibu na uke.

Makala zaidi: Usiyoyajua Kuhusu Ugonjwa wa PID: Dalili 7 za pid Za Mapema.
3.Je! Rangi za kutokwa na uchafu ukeni zinamaanisha nini?
- Njano, kijivu au kijani: Inaweza kuwa ishara ya maambukizi ya bakteria au magonjwa ya zinaa (STI).
- Kahawia au nyekundu: Mara nyingi huhusishwa na hedhi isiyo ya kawaida au ujauzito (kutokwa damu ya upandikizaji mimba). Ikiwa Unatokwa nah ii na si kipindi chako cha hedhi, inaweza kuashiria tatizo Fulani kwenye kizazi.
- Uchafu angavu (Clear) au mweupe: Ni kawaida. Hata hivyo, kama ni mzito zaidi ya kawaida (kama mtindi) au unasababisha kuwashwa, inaweza kuwa fangasi (yeast infection).
- Wasiliana na daktari ikiwa uchafu wako unabadilika rangi, muundo, au unaambatana na harufu kali, Uchafu wa kuwashwa au kuchoma choma.
4.Je, mabadiliko katika uchafu wa ukeni ni dalili ya maambukizi?
- Inawezekana. Unaweza kugundua mabadiliko katika rangi, harufu au kiasi. Kuwashwa kwenye mlango wa uke pia kunaweza kutokea. Mabadiliko haya yanaweza kutokea kabla au baada ya hedhi. Kama huna uhakika, ni vyema kumwona mtaalamu wa afya.
Je, unaweza kupata maambukizi ya ukeni zaidi ya aina moja kwa wakati mmoja?
- Ndiyo. Inawezekana kuwa na aina mbili au tatu za maambukizi kwa wakati mmoja.

Makala zaidi: Dawa ya Tumbo la Hedhi – Namna ya Kupona Kabisa
5.Sababu za kutoka uchafu mweupe ukeni na Rangi zingine.
- Maambukizi yanayosababisha mabadiliko:
- Fangasi (Yeast Infection):
Fangasi wa aina ya Candida huzaliana kupita kiasi ukeni na kusababisha uchafu mzito mweupe kama jibini (maziwa mtindi). Uke huvimba, kuwasha, na kufanya tendo la ndoa kuwa chungu (maumivu wakati wa tendo la ndoa). Tiba zake ni dawa za kuua fangasi. - Trikomonasi (Trichomoniasis au “Trich”):
Maambukizi haya husababishwa na parasaiti na huambukizwa kwa ngono. Uchafu huwa wa rangi ya kijani, rangi ya njano au rangi ya kijivu, uchafu wenye povu. Tiba zake ni antibiotiki. - Bacterial Vaginosis (BV):
Hutokea pale ambapo kuna ongezeko la aina fulani ya bakteria ukeni. Inaweza kuwa kupitia ngono au bila ngono. Uchafu huwa mweupe au kijivu na huambatana na harufu ya samaki. Tiba zake zilizozoeleka ni antibiotiki. - Gonorrhea na Chlamydia:
Magonjwa haya huambukizwa kwa ngono. Watu wenye maambukizi haya huweza kuwa na uchafu wa rangi ya njano, rangi ya kijani au rangi ya mawingu. Maambukizi haya yakiendelea Bila tiba, yanaweza kusababisha ugonjwa wa maambukizi kwenye kizazi (pelvic inflammatory disease - PID).

Makala zaidi: Zijue dalili za mimba changa | Dalili 12 za awali.
6.Sababu zisizotokana na maambukizi:
- Kitu kisicho cha kawaida ndani ya uke (k.m. tamponi iliyosahaulika).
- Kuwashwa au mzio kutokana na sabuni, vilainishi, kondomu au vitu vya kutumia wakati wa tendo la ndoa.
- Atrophic vaginitis: Hii hutokea Baada ya kukoma kwa hedhi (menopause), Kutokana na viwango vya estrojeni hushuka, na kuta za uke kuwa kavu na nyembamba.
- Kuwa na Ujauzito: Mwili huzalisha uchafu zaidi ili kujilinda dhidi ya maambukizi.
- Kipindi cha Ovulation: Uchafu huwa mwingi na wenye mtelezo kusaidia mbegu za kiume kusafiri kwa urahisi kuelekea kwenye yai.
Kwa nini huwa Unapatwa hali ya kutokwa na uchafu ukeni kila siku?
- Ni kawaida kabisa (Kama hauna harufu wala rangi). Huwezi kuuzuia kwa sababu ni njia ya mwili kujisafisha na kujilinda. Kama unaona ni mwingi sana, unaweza kutumia panty liner kunyonya unyevu huo.
Vipi kama upo na Ujamzito – je, uchafu hubadilika?
- Ndiyo, ni kawaida kuwa na uchafu mwingi zaidi wakati wa ujauzito. Kwa sababu Homoni kama progesterone huongeza uzalishaji wa uchafu (Uteute). Uchafu huu husaidia kulinda dhidi ya maambukizi yanayoweza kufika kwenye mfuko wa mimba. Wasiliana na daktari wa wajawazito endapo kutakuwa na mabadiliko yasiyo ya kawaida kwenye uchafu unaotoka ukeni.
Kwa nini uchafu wangu unanuka (Unatoa harufu)?
- Harufu mbaya inaweza kuwa ishara ya maambukizi, hasa kama ni kali au kama ya samaki. Ni vyema kupimwa mapema ili kupata tiba.
Kwa nini wengi hupata maambukizi ya ukeni?
- Wataalamu bado hawajafahamu kwa kina sababu zote, lakini baadhi ya vitu vinavyochangia ni Hivi hapa:
- Kufanya ngono bila kinga au kuwa na wapenzi wengi.
- Kuwa na Kisukari kisichodhibitiwa vizuri.
- Matumizi ya vidonge vya uzazi wa mpango.
- Kutumia dawa za antibiotiki.
- Maambukizi ya HIV au Kuwa na kinga iliyo dhaifu.
- Matumizi ya sabuni au dawa zenye kemikali kali.
- Kujisafisha kwa njia ya douching (kuosha uke kwa maji kwa kujichokonoa kwa ndani).