- Ugonjwa wa PID (Pelvic Inflammatory Disease) ni tatizo linalowakumba wanawake wengi duniani, hasa walio katika umri wa kuzaa. Huu ni ugonjwa wa maambukizi katika viungo vya uzazi vya ndani kama vile mfuko wa uzazi (uterasi), mirija ya uzazi (fallopian tubes), na ovari. Ugonjwa huu huweza kuathiri sana afya ya uzazi ikiwa hautatibiwa mapema.
- Katika makala hii, tutazungumzia kwa kina dalili za PID, sababu zake, tiba inayopatikana, na mbinu 6 muhimu za kuzuia maambukizi haya. Lengo ni kukupa maarifa sahihi ili uweze kujilinda na pia kusaidia wengine katika jamii yako.

Makala zaidi: Tatizo la kutoshika mimba: Sababu na Tiba zake za Haraka.
Ugonjwa wa PID ni nini?
- PID ni kifupi cha "Pelvic Inflammatory Disease", yaani ugonjwa wa kuambukiza unaoathiri sehemu ya ndani ya via vya uzazi vya mwanamke. Ugonjwa huu mara nyingi husababishwa na bakteria, hasa wale wanaosababisha magonjwa ya zinaa kama vile Chlamydia na Gonorrhea. Bakteria hawa huingia kupitia shingo ya kizazi (cervix) na kupanda hadi kwenye mfuko wa uzazi na mirija ya uzazi.
Dalili za PID Muhimu Kuzingatia.
- Ni muhimu kuzitambua dalili za PID mapema ili kupata matibabu haraka. Dalili zinaweza kuwa nyepesi au kali kulingana na kiwango cha maambukizi. Hizi hapa ni dalili za kawaida:
- Maumivu ya tumbo la chini ya kitovu
- Maumivu wakati wa tendo la ndoa
- Kutokwa na uchafu usio wa kawaida ukeni (unaonuka au wenye rangi tofauti)
- Homa na baridi kali
- Maumivu wakati wa kukojoa
- Kuingiliwa kwa hedhi (bleeding) bila sababu maalum, hasa baada ya tendo la ndoa
- Uchovu usioelezeka
- Ikiwa unapata mojawapo ya hizi dalili za PID, ni vyema kumwona daktari mara moja kwa uchunguzi na matibabu.

Makala zaidi: Ili kupona vidonda vya tumbo-Suluhisho bora ni hili Hapa.
Sababu za Ugonjwa wa PID
Kuna mambo mbalimbali yanayoweza kuongeza hatari ya kupata ugonjwa wa PID. Hizi ndizo sababu kuu:
- Kufanya ngono bila kinga na watu tofauti
- Kuambukizwa magonjwa ya zinaa (STIs)
- Kutumia vifaa vya kuzuia mimba kama IUD (hasa katika siku za mwanzo baada ya kuwekwa)
- Historia ya PID hapo awali
- Douching (kusafisha uke kwa kutumia dawa au maji ya shinikizo)
Kufahamu sababu hizi hukusaidia kuchukua hatua za kuzuia maambukizi kabla hayajatokea.

Makala zaidi: Maumivu ya tumbo la hedhi (Dysmenorrhoea | chango la uzazi
Madhara ya PID Ikiwa Haitatibiwa
Ugonjwa wa PID usipotibiwa mapema unaweza kusababisha madhara makubwa kwa afya ya uzazi:
- Ugumba (kutopata mimba)
- Mimba kutunga nje ya mfuko wa uzazi (ectopic pregnancy)
- Maumivu sugu ya nyonga
- Uharibifu wa mirija ya uzazi
- Kuathirika kwa maisha ya ndoa na mahusiano
Ndiyo maana ni muhimu kutambua dalili mapema na kufuata matibabu sahihi.
Tiba ya PID
- Matibabu ya ugonjwa wa PID yanahusisha matumizi ya antibiotiki zinazopambana na bakteria walioleta maambukizi. Mgonjwa anaweza kupewa dawa ya kumeza au sindano kulingana na hali yake. Mara nyingine, kulazwa hospitalini huhitajika ikiwa maambukizi ni makali sana.
- Wakati mwingine, upasuaji unaweza kuwa muhimu iwapo kuna usaha au uharibifu mkubwa kwenye via vya uzazi.
- Ni muhimu sana kumaliza dozi ya dawa hata kama dalili zimepungua, ili kuhakikisha bakteria wote wamekufa kabisa. Pia, mwenza wa kimapenzi anapaswa kutibiwa ili kuzuia maambukizi kurudi tena.

Makala zaidi: Tatizo la kutoshika mimba: Sababu na Tiba zake za Haraka.
Suluhisho la Asili kwa Tatizo Sugu la PID Sugu
- Kama tatizo lako limekuwa kubwa, na umetumia dawa nyingi bila mafanikio, usikate tamaa! Sasa kuna suluhisho la asili ambalo limethibitishwa kusaidia wanawake wengi waliokuwa katika hali kama yako. Tumia dawa maalumu ya asili – STD CARE.
- STD CARE ni tiba ya asili iliyotengenezwa kwa mimea tiba yenye nguvu ya kuondoa bakteria wanaosababisha PID, ikilenga mzizi wa tatizo. Dawa hii:
- Huondoa kabisa maambukizi sugu ya PID
- Husaidia kurejesha afya ya via vya uzazi na kuondoa maumivu
- Huzuia maambukizi kujirudia tena
- Haina madhara kwa mwili kwa kuwa ni ya asili kabisa
Inafaa sana kwa wanawake waliochoka kutumia dawa za kila mara bila mafanikio ya kudumu. Imeonyesha mafanikio makubwa kwa wagonjwa waliokuwa wamekata tamaa.
- Kwa ushauri wa kitaalamu au kupata STD CARE, unaweza kuwasiliana nasi moja kwa moja kwa maelekezo ya matumizi na namna ya kuipata. Piga simu au Whatsapp 0745 889 503 au 0711 556 377
Njia 6 za Kuzuia Ugonjwa wa PID
- Tumia kondomu kila mara unapofanya ngono – hii ni njia bora zaidi ya kujikinga na magonjwa ya zinaa.
- Epuka kubadilisha wapenzi mara kwa mara – kuwa na uhusiano wa kudumu husaidia kupunguza hatari.
- Pima afya mara kwa mara – hasa ikiwa una mahusiano ya kimapenzi, ni vizuri kupima STIs kwa wakati.
- Epuka douching (Kujichokonoa ukeni)– husababisha kuondoa bakteria wazuri wanaolinda uke.
- Hudhuria kliniki mara baada ya kuona dalili yoyote isiyo ya kawaida – usisubiri hali kuwa mbaya zaidi.
- Shirikiana na mwenza wako kwenye suala la afya yako ya uzazi – Elimu ya pamoja na mawasiliano Bora ya wapenzi husaidia sana.
Hitimisho
- Ugonjwa wa PID ni changamoto kubwa kwa afya ya uzazi ya wanawake, lakini ni ugonjwa unaoweza kuzuilika na kutibika kabisa ikiwa utachukuliwa kwa uzito. Kutambua mapema dalili za PID, kufuata matibabu kwa usahihi, na kuchukua tahadhari ni hatua muhimu za kulinda afya yako ya uzazi.
- Jilinde leo, elimisha wengine, na weka afya yako ya uzazi kuwa kipaumbele Bora!