Ugonjwa wa kisukari | Dalili 8 na Madhara yake

Ugonjwa wa kisukari ni ugonjwa miongoni mwa magonjwa sugu yanayoathiri watu wengi sana siku hizi hapa duniani, Hii hasa Ni kutokana na mtindo wa maisha Wa watu wengi Kuwa wa kisasa. Katika makala hii, tutaelezea kwa undani Kuhusu ugonjwa huu wa kisukari Kwamba  unasababishwa na nini, dalili zake ni zipi, madhara yake yapoje , na dawa asili ya Kuweza kumaliza  ugonjwa huu wa kisukari Bila Kujirudia. Dawa ambayo imekuwa msaada mkubwa kwa watu wengi waliosumbuliwa na Tatizo hili kwa muda Mrefu sana.

ugonjwa wa kisukari

Makala zaidi: Dawa za kisukari tanzania | Diabetic Care-Dawa Asili

Bila kupoteza muda fuatana nami Hatua kwa hatua Tunapoanza kuchambua hoja moja baada ya nyingine.

Ugonjwa wa Kisukari Unasababishwa na nini?

Ugonjwa huu wa Kisukari ni ugonjwa unaotokea Kuanzia pale ambapo mwili unakuwa katika hali ya kushindwa kudhibiti viwango vya sukari (glucose) katika damu. Hivyo kupelekea Kuwepo na kiwango kikubwa cha sukari kwenye damu (Hyperglycaemia). Hata hivyo Kuna aina kuu tatu za Ugonjwa wa kisukari:

ugonjwa wa kisukari unasababishwa na nini

Makala zaidi: A-Z Kuhusu Ugonjwa wa kisukari | Sababu, na Dalili zake

  1. Ugonjwa wa Kisukari Aina ya Kwanza (Type 1 Diabetes)
    Aina hii ya kisukari hutokea pale ambapo kiungo cha kongosho hushindwa kabisa kuzalisha homoni ya insulini. Aina hii ya kisukari Hutokea kwa Sababu za kurithi au Kutokana na mfumo wa kinga ya mwili Kuanza kushambulia seli za kongosho, ambazo huhusika na uzalishaji wa homoni ya insulini.
  • Aina Hii ya kisukari pia hujulikana kama kisukari cha Utotoni (Childhood onset diabets) Kisukari cha kuzaliwa nacho au kisukari cha utotoni (Juvenile Diabetes)
wasiliana na doctor online

2. Kisukari Aina ya Pili (Type 2 Diabetes)
Kisukari cha aina ya pili pia hujulikana kama Kisukari cha ukubwani (Adult onset Diabetes)

  • Aina hii ndiyo huapata watu wengi sana na huhusiana sana na Kuwa na uzito mkubwa, Hali ya kutofanya mazoezi, na Hutokana na  lishe mbaya (Mlo wa kimagharibi).
  • Mtu mwenye aina hii ya kisukari Mwili wake hushindwa kutumia vizuri homoni ya insulini ambayo tayari imezalishwa (Insulin Resistance) au Mara chache kongosho yake hushindwa kuzalisha insulini ya kutosha.
Ugonjwa wa kisukari dalili zake

Makala zaidi: Dawa ya nguvu za kiume Ya Haraka | SUPER MULTI-PLUS

Ugonjwa wa kisukari dalili zake.

Dalili za kisukari zinaweza kufanana au kutofautiana kulingana na aina ya kisukari. Kama tunavyojua kuna kisukari cha aina 2 Aina ya Kwanza (Type 1) na Aina ya Pili (Type 2). Japo  Dalili zinaweza kufanana, lakini pia hutofautiana kwa kiwango fulani  na kasi ya kuanza kwake. Hapa kuna dalili ambazo ni za kawaida za kisukari kwa aina zote:

wasiliana na doctor online

Dalili Kuu za Kisukari aina ya kwanza & Ya Pili (Type 1 na Type 2):

  • Hali ya Kukojoa mara kwa mara (polyuria)
  • Hali ya Kupata Kiu kupita kiasi (polydipsia)
  • Hali ya Kupata Njaa kupita kiasi (polyphagia)
  • Hali ya Kupungua uzito ghafla bila sababu ya msingi (hasa Type 1)
  • Kuwa na Uchovu au Hali ya kuishiwa nguvu.
  • Hali ya Kuona ukungu (blurred vision) & Uoni Hafifu
  • Hali ya Vidonda au michubuko inayopona polepole (Kupona kwa shida)
  • Kupata Maambukizi ya mara kwa mara, kama vile maambukizi ya ngozi au maambukizi sehemu za siri.
Ugonjwa wa kisukari dalili zake kuu

Makala zaidi: Tatizo la kutoshika mimba: Sababu na Tiba  zake za Haraka.

Dalili za Kisukari Aina ya Kwanza (Type 1) Diabetes

  • Dalili Za hapo juu huanza ghafla na kwa kasi Kubwa.
  • Hupelekea Kupungua kwa uzito kwa haraka.
  • Kupata hali ya Ketoacidosis (hali hatari inayosababishwa na ukosefu wa insulini), huweza kusababisha kichefuchefu Kikali, kutapika, maumivu ya tumbo, Kupumua pumzi kama harufu ya matunda.
  • Kuishiwa nguvu na kuzimia.
wasiliana na doctor online

Dalili za Kisukari Aina ya Pili (Type 2 Diabetes)

  • Dalili huanza polepole na unaweza usizitambue mapema.
  • Kuwa na Hali ya ganzi au kufa ganzi mikononi au miguuni (Peripheral neuropathy)
  • Kupata Maambukizi ya mara kwa mara, hasa hasa fangasi sehemu za siri.
  • Kupata hali Ukosefu wa nguvu za kiume (kwa wanaume)
  • Kupata Mabadiliko kwenye ngozi (dark patches, hasa shingoni au kwapani – acanthosis nigricans)

Zingatia Kuwa : Wengine huwa hawana dalili zozote kabisa mwanzoni, hasa wagonjwa wenye Type 2, na hujulikana tu baadae wakati wa vipimo vya afya kwa sababu za nyingine tu.

ugonjwa wa kisukari Madhara yake

Makala zaidi: Jinsi ya Kushinda Ugonjwa wa P i d: Sababu, Tiba na Njia 6 za Kujikinga kwa Mafanikio

Ugonjwa wa kisukari Madhara yake

Madhara ya Muda Mrefu (Chronic Complications)

Madhara Haya hujitokeza baada ya miaka mingi ya kuwa na kisukari kisichodhibitiwa:

wasiliana na doctor online

1.Madhara kwa Afya ya Moyo na Mishipa ya Damu:

  • Kufanya Presha ya damu kuwa juu (high blood pressure)
  • Kuongeza Hatari ya kupata tatizo la mshituko wa moyo (heart attack)
  • Kuongezeka hatari ya kupata kiharusi Kiharusi (stroke)
  • Tatizo la Atherosklerosisi – mishipa kuziba kwa mafuta

2.Madhara kwa Afya ya Macho (Diabetic Retinopathy):

Madhara ya kisukari kwenye macho
  • Kuendelea Kupungua kwa uwezo wa kuona
  • Hatimaye kupata upofu

3.Madhara katika  Mishipa ya Fahamu (Diabetic Neuropathy):

  • Kuwa na Maumivu, Kuhisi ganzi au kufa ganzi kwenye miguu/mikono
  • Hisia Za miguuni au mikononi kuwa dhaifu
  • Kujikata bila kujua.
wasiliana na doctor online

4.Madhara kwa Miguu:

  • Kuwa na Vidonda visivyopona kwa urahisi (diabetic foot ulcers)
  • Kuongezeka kwa Hatari ya kupelekea kukatwa mguu (amputation)

5. Madhara kwa Afya ya Figo (Diabetic Nephropathy):

madhara ya kisukari kwenye figo
  • Huongezeka kwa hali ya Kushindwa kwa figo kufanya kazi
  • Kupelekea Uhitaji wa Kufanyiwa dialysis kila mara au Kupandikiziwa figo.

6. Madhara kwa Upande wa Kinga ya Mwili:

  • Hali ya kupata Maambukizi ya mara kwa mara
  • Kupata Fangasi na bakteria sehemu za siri, mdomoni, na kwenye ngozi ngozi.
wasiliana na doctor online

2. Madhara ya Muda Mfupi (Acute Complications)

Sukari kuwa juu sana * (Hyperglycemia):*

  • Hali inayopelekea Kuchanganyikiwa, kupata kiu kiu kali, kupata kukojoa sana, hasa usiku.
  • Hali hii Inaweza kusababisha hali ya hatari zaidi kama vile ketoacidosis (hasa kwa wenye Type 1 Diabetes)

Sukari kushuka sana  (Hypoglycemia):

  • Hali ambayo hupelekea Kutetemeka, Kutokwa jasho, na kupata kizunguzungu
  • Hali ya Kuanguka au hata kupoteza fahamu
  • Kwa kawaida Hali hii inaweza kuhatarisha maisha ya mgonjwa.

Madhara kwa Afya ya Uzazi (Kwa Wanawake na Wanaume):

  • Kupata Ugumba au Kupata  matatizo katika kushika mimba.
  • Kuongezeka kwa hatari ya kuzaa mtoto mkubwa,mwenye kichwa kikubwa au Kuongezeka kwa matatizo wakati wa kujifungua (Kifafa cha mimba, na Kujifungua kwa operation kutokana na mtoto kubwa kushindwa kupita kawaida)
  • Tatizo la nguvu za kiume kwa wanaume
wasiliana na doctor online

Ufumbuzi:

Katika Madhara haya mengi kati yake yanaweza kuzuilika au kucheleweshwa sana kwa kufanya yafuatayo:

  • Kufuata  Mpango wa lishe bora
  • Kushirika katika Kufanya mazoezi mara kwa mara (Kila siku)
  • Kuendelea kutumia  dawa za kisukari kama ulivyoelekezwa na dakitari.
  • Kudhibiti msongo wa mawazo (stress)
  • Kufuatilia kwa karibu kiwango cha sukari mara kwa mara.

Je ungependa kupata Tiba ya kumaliza kabisa tatizo la kisukari na kuweza kuishi maisha ya kawaida kama watu wengine? Kuna mpango Bora wa Tiba na Lishe utaomaliza kabnisa tatizo lako, Tuma neno KISUKARI Kwenda namba 0711556377 Upate mwongozo wa Kufaa kumaliza tatizo hili.

wasiliana na doctor online

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *