Saratani ya Kizazi (mji wa uzazi)(Uterine Cancer / Endometrial Cancer)
Saratani ya Kizazi (mji wa uzazi)ni aina ya saratani inayotokea kwenye Kizazi (mji wa uzazi)wa mwanamke. Kuna aina mbili:
Endometrial cancer,inayotokea kwenye ukuta wa ndani wa mji wa mimba (endometrium). Hii ndiyo aina inayotokea kwa asilimia 95 ya wagonjwa.
Uterine sarcoma, saratani adimu inayotokea kwenye misuli ya mji wa uzazi.
Kazi ya Mji wa Uzazi
Kizazi (mji wa uzazi)ni sehemu ambapo mimba hukua. Sehemu ya juu huitwa “corpus” na sehemu ya chini huungana na shingo ya uzazi (cervix). Saratani ya Kizazi (mji wa uzazi)hutokea kwenye sehemu ya juu (corpus), na siyo kwenye shingo ya kizazi.
Kazi ya Endometrium
Endometrium hubadilika kulingana na mzunguko wa hedhi. Homoni za estrogeni na projesteroni huufanya ukuta wa ndani unene kwa maandalizi ya ujauzito. Ujauzito usipotokea, ukuta huu huondoka kama hedhi.
Saratani ya Kizazi (mji wa uzazi) Huonekana Mara ngapi?
Ni saratani ya kawaida kwa wanawake waliomaliza hedhi, na takribani asilimia 3 ya wanawake hupata tatizo hili katika maisha yao.
Dalili za Saratani ya Mji wa Uzazi
Dalili zake zinaweza kufanana na magonjwa mengine ya uzazi, hivyo uchunguzi wa daktari ni muhimu.
Kutokwa na damu katikati ya mzunguko kabla ya hedhi kukoma.
Kutokwa na damu hata kidogo baada ya kukoma hedhi.
Maumivu ya tumbo la chini au kukaza kwenye nyonga.
Wakati mwingine ute mweupe au maji kutoka ukeni kwa wanawake waliokoma hedhi.
Hedhi nzito kupita kawaida kwa wanawake zaidi ya miaka 40.
Visababishi na Vihatarishi
Chanzo halisi hakijulikani, lakini seli hubadilika na kuanza kukua bila mpangilio.
Vihatarishi muhimu:
- Umri
Hatari huongezeka baada ya miaka 50. - Unene (Obesity)
Mafuta mwilini huzalisha estrogeni nyingi, jambo linaloongeza hatari. - PCOS
Wanawake wenye polycystic ovarian syndrome huwa na homoni zisizo sawa, hivyo hatari huongezeka. - Kisukari
Hata bila unene, kisukari kinaweza kuongeza hatari. - Historia ya Familia
Hasa wenye Lynch syndrome. - Matumizi ya Estrogeni Pekee
Kutumia estrogeni bila projesteroni (HRT) huongeza hatari. - Hedhi za Mapema na Kukoma kwa Hedhi kwa Baadaye
Hedhi kuanza kabla ya miaka 12
Kukoma kwa hedhi baada ya miaka 50 - Kutopata Mtoto
Wanawake ambao hawajawahi kushika mimba wako kwenye hatari zaidi. - Tiba za Awali
Tiba ya mionzi kwenye nyonga
Matumizi ya tamoxifen kwa wagonjwa wa saratani ya matiti
Vipimo na Uchunguzi
Daktari anaweza kufanya vipimo vya:
- Vipimo vya damu
Kipimo cha CA-125 (huongezeka kwa baadhi ya wagonjwa). - Vipimo vya picha
Ultrasound ya kupitia uke
CT-scan
MRI - Vipimo vya kuchukua sampuli
Endometrial biopsy (kifaa kidogo kinapitishwa kupitia mlango wa uzazi kuchukua tishu)
Hysteroscopy (kamera ndogo inaingizwa ukeni kutazama ndani)
Dilation and Curettage (D&C) – hufanywa hospitalini.
Kumbuka: Pap smear haigundui saratani ya mji wa uzazi; kazi yake ni kugundua saratani ya shingo ya kizazi.
Aina na Hatua za Saratani
Saratani hupangwa kulingana na kasi yake:
Type 1 – ya kawaida, hukua polepole
Type 2 – ya ukali zaidi, huhitaji matibabu makali
Hatua za Saratani (Stages I–IV)
Stage I: Iko ndani ya mji wa uzazi
Stage II: Imefika kwenye shingo ya uzazi
Stage III: Imeenea kwenye uke, ovari au tezi za limfu
Stage IV: Imeenea mbali, mfano kibofu au viungo vingine
Matibabu
Matibabu hutegemea hatua ya ugonjwa, aina ya saratani na afya ya mgonjwa.
- Upasuaji (Surgery)
Ndiyo matibabu ya msingi kwa karibu wagonjwa wote.
Aina za upasuaji:
Total abdominal hysterectomy hii ni hatua ya kuondoa Kizazi (mji wa uzazi)kwa kufungua tumbo.
Vaginal hysterectomy hii kuondoa kupitia uke.
Radical hysterectomy hii hutolewa hutolewa pia tishu za pembeni na sehemu ya juu ya uke ikiwa saratani imeenea.
Minimally invasive surgery hutolewa kwa kutumia tundu dogo (laparoscopy/robotic).
Mara nyingi huambatana na:
Kuondoa ovari na mirija (BSO)
Kuondoa tezi za limfu (lymphadenectomy) - Mionzi (Radiation Therapy)
Huteketeza seli za saratani. - Chemotherapy
Dawa kali zinazoangamiza seli za saratani. - Tiba ya Homoni
Huzuia au kupunguza homoni zinazoifanya saratani kukua. - Immunotherapy
Huchochea kinga ya mwili kupambana na saratani. - Targeted Therapy
Hume-target seli maalum za saratani bila kuathiri seli nzima mwilini.
Matokeo na Utabiri (Prognosis)
Survival rate (miaka 5): 81%
Ikigunduliwa mapema: hadi 95%
Ikienea mbali: inashuka hadi 17%
Ugunduzi wa mapema huongeza sana uwezekano wa kupona.
Kinga (Prevention)
Ingawa haiwezi kuzuilika kikamilifu, unaweza kupunguza hatari kwa:
Kudhibiti uzito
Kuwa na lishe bora
Kudhibiti kisukari
Kutumia dawa za uzazi zenye mchanganyiko wa estrogen + projesteroni (hutoa ulinzi fulani)
Kuepuka matibabu ya estrogeni pekee bila ushauri
Hakuna kipimo maalum cha uchunguzi wa mapema kwa wanawake wasio na dalili, isipokuwa kwa wale walio kwenye hatari kubwa kama wenye Lynch syndrome.
Maisha Baada ya Matibabu
Ni muhimu kufuata miadi ya daktari kwa:
Uchunguzi wa nyonga
Kuangaliwa dalili zozote zinazoweza kuashiria kurudi kwa saratani
Ushauri wa lishe, mazoezi na usaidizi wa kihisia
Maswali Muhimu kwa Daktari Wako
Hatua ya saratani yangu ni ipi?
Ni matibabu gani yanafaa kwangu?
Je, nitahitaji mchanganyiko wa matibabu?
Je, kuna clinical trials?
Natarajia nini baada ya matibabu?
Je, saratani inaweza kurudi?
Maswali ya Kawaida (FAQ)
Dalili za onyo ni zipi?
Kutokwa na damu isiyo ya kawaida hasa baada ya kukoma hedhi.
Saratani ya Kizazi (mji wa uzazi)huenea kwa kasi?
Type 1: polepole
Type 2: kwa kasi zaidi
Hutokea kwa umri gani zaidi?
Kwa wanawake waliomaliza hedhi, wastani miaka 51.