SARATANI NI NINI?

Saratani ni ugonjwa unaotokea pale ambapo baadhi ya seli za mwili zinakua bila mpangilio, haziishi wakati zinapaswa kufa, na zinaweza kuenea kwenye sehemu nyingine za mwili.


Kwa kawaida, seli za mwili hukua na kuzaliana kulingana na mahitaji ya mwili. Zikizeeka au kuharibika, zinakufa na nafasi yake kuchukuliwa na seli mpya. Lakini katika saratani, mchakato huu unavurugika na seli zisizo za kawaida huanza kuzaliana kupita kiasi.
Seli hizi zinaweza kutengeneza uvimbe (tumor).
Uvimbe mwovu (malignant):

Unaenea na kuvamia tishu nyingine.
Uvimbe usio wa saratani (benign):

Hauenei katika tishu jirani, ingawa unaweza kukua na kuwa mkubwa.


Baadhi ya saratani, kama zile zinazoathiri damu (mfano leukemia), hazitengenezi uvimbe wa kawaida.
Tofauti za kibiologia kati ya seli za kawaida na seli za saratani.
Seli za saratani hutofautiana na seli za kawaida kwa namna kadhaa:
Hukua bila kuhitaji ishara za ukuaji.
Hupuuza ishara zinazotakiwa kuzizuia kugawanyika.
Huendelea kukua hata zinapogusana na seli nyingine, wakati seli za kawaida husimama.
Huwa na uwezo wa kuvamia maeneo ya karibu na kusambaa mwilini.
Huvutia mishipa ya damu kuja kwenye uvimbe ili kupata virutubisho.
Hujiwekea njia za kujificha dhidi ya kinga ya mwili.
Huwa na mabadiliko mengi ya vinasaba (DNA), kama kurudiwa kwa sehemu za kromosomu au kupungua.
Hutumia nishati kwa njia isiyo ya kawaida ili ziweze kukua haraka.
Kwa sababu hizi, watafiti hutengeneza tiba zinazoilenga tabia hizi za kipekee za seli za saratani kama tiba zinazoizuia mishipa ya damu kupeleka virutubisho kwenye uvimbe.

Saratani huanza Kwa namna gani?
Saratani ni ugonjwa wa kijenetiki, ikimaanisha inasababishwa na mabadiliko kwenye vinasaba vinavyodhibiti ukuaji na mgawanyiko wa seli.
Mabadiliko haya ya vinasaba yanaweza kutokea kwa sababu ya:
Makosa wakati seli zinajigawanya
Uharibifu wa DNA kutokana na mazingira (mfano jua kali, kemikali, moshi wa sigara)
Kurithi mabadiliko ya kijeni kutoka kwa wazazi
Mara nyingi mwili huondoa seli zenye DNA iliyoharibika, lakini uwezo huu hupungua kadri tunavyozeeka, jambo linaloongeza hatari ya saratani.
Kila saratani ina mchanganyiko wake wa kipekee wa mabadiliko ya vinasaba, na hata ndani ya uvimbe mmoja, seli tofauti zinaweza kuwa na tofauti za kijeni.
Aina za Vinasaba vinavyohusishwa na Saratani.
Mabadiliko ya DNA katika saratani huathiri hasa makundi matatu ya vinasaba:

  1. Proto-oncogenes
    Husaidia seli kukua kwa kawaida. Zikiharibika, hugeuka kuwa oncogenes, zinazochochea ukuaji usio na kikomo.
  2. Tumor suppressor genes
    Hukazia ukuaji wa seli au kuziua zinapoharibika. Zikifeli, seli hukua bila kudhibitiwa.
  3. DNA repair genes
    Hurekebisha makosa kwenye DNA. Zinapoharibika, seli hubeba makosa mengi zaidi na kugeuka saratani kwa urahisi.
    Uelewa wa mabadiliko haya umewezesha wataalamu kubuni tiba zinazoilenga saratani kulingana na mabadiliko maalum ya kijeni, bila kujali saratani ilianzia wapi.
    Saratani Inaposambaa (Metastasis)
    Saratani inaposambaa kutoka sehemu ilipoanzia kwenda sehemu nyingine ya mwili, huitwa metastasis.
    Mfano: Saratani ya matiti ikisambaa hadi kwenye mapafu bado huitwa saratani ya matiti.
    Saratani inayosambaa mara nyingi ndiyo huua wagonjwa wengi kwa sababu inaathiri kazi muhimu za mwili.
    Madaktari hujalibu:
    Kuzuia kuenea kwa saratani
    Kupunguza dalili
    Kurefusha maisha
    Mabadiliko ya Tishu Ambayo Sio Saratani
    Baadhi ya mabadiliko ya tishu siyo saratani, lakini yanaweza kupelekea saratani ikiwa hayataangaliwa:
  4. Hyperplasia
    Kuongezeka kwa idadi ya seli lakini muundo bado unaonekana wa kawaida.
  5. Dysplasia
    Seli huonekana zisizo za kawaida na muundo wa tishu hubadilika. Inaweza kuendelea kuwa saratani.
  6. Carcinoma in situ
    Hii ni hatua ya juu zaidi ya mabadiliko—sio saratani kamili kwa sababu seli hazijavunja ukuta wa tishu, lakini mara nyingi hutibiwa ili isigeuke saratani.
    Aina Kuu za Saratani
    Kuna zaidi ya aina 100 za saratani. Hapa ni makundi makuu:
  7. Carcinoma
    Hutokana na seli za epithelial (zinazofunika ndani na nje ya mwili).
    Aina zake ni pamoja na:
    Adenocarcinoma hutokea kwenye matiti, tezi dume, utumbo
    Basal cell carcinoma hutokea kwenye ngozi
    Squamous cell carcinoma hutokea katika ngozi, mapafu, tumbo
    Transitional cell carcinoma hutokea katika kibofu cha mkojo
  8. Sarcoma
    Hutoka kwenye mifupa na tishu laini kama misuli, mafuta, mishipa ya damu, na tishu unganishi.
  9. Leukemia
    Hutokea kwenye uboho na huongezeka kwenye damu badala ya kutengeneza uvimbe.
  10. Lymphoma
    Huanza kwenye lymphocytes (seli za kinga).
    Aina mbili kuu:
    Hodgkin lymphoma
    Non-Hodgkin lymphoma
  11. Multiple Myeloma
    Huanza kwenye plasma cells zinazozalisha kinga mwilini.
  12. Melanoma
    Saratani ya melanocytes (seli zinazotengeneza rangi ya ngozi).
  13. Tumors za Ubongo na Uti wa Mgongo
    Zinategemea aina ya seli ya ubongo iliyoathirika.
  14. Germ Cell Tumors
    Huanza kwenye seli za uzazi (mbegu na yai).
  15. Neuroendocrine Tumors
    Hutokana na seli zinazotengeneza homoni.
  16. Carcinoid Tumors
    Aina ya neuroendocrine tumor, mara nyingi kwenye mfumo wa chakula.