uvimbe kwenye kizazi

Tatizo la Uvimbe kwenye kizazi ( Uterine Fibroids).

Uterine fibroids ni uvimbe wa kawaida unaokua kwenye mfuko wa uzazi usiokuwa wa saratani. Mara nyingi uvimbe huu hujitokeza katika miaka ya uwezo wa kushika mimba na kujifungua. Hii Si kansa, na mara nyingi vimbe hizi kamwe haviwezi kuwa kansa.

Pia havihusiani na hatari kubwa ya aina nyingine za saratani ya mfuko wa uzazi, hadi pale panapokuwapo na Hatari zingine nyingi zaidi. Uvimbe kwenye kizazi (Fibroids) pia huitwa leiomyomas au myomas.

Fibroids hutofautiana kwa idadi na ukubwa: unaweza kuwa na uvimbe mmoja au vimbe nyingi kwa pamoja. Baadhi huwa ni vidogo sana, vingine hukua hadi kufikia ukubwa wa chungwa kubwa au zaidi, na vinaweza kuwa vikubwa sana hadi kupindisha umbo la mfuko wa uzazi.

Katika hali kali mno, vinaweza kujaza nyonga au tumbo na kumfanya mtu aonekane kama mjamzito.

Watu wengi huwa wana fibroids wakati fulani wa maisha, lakini mara nyingi hawajui kwa kuwa havileti dalili yoyote ya wazi. Mara nyingi hugundulika tu wakati wa uchunguzi wa vipimo vya nyonga au ultrasound ya ujauzito.

uvimbe kwenye kizazi.

Makala zaidi: Dawa ya uvimbe kwenye kizazi Bila Upasuaji

1.Dalili za uvimbe kwenye kizazi

Watu wengi japo huwa hawana dalili mwanzoni. Lakini  wanapokuja kupata dalili, hutegemea mahali uvimbe ulipo, ukubwa wake na idadi ya hizo fibroids.

Dalili za kawaida ni:

  • Kutokwa na damu nyingi wakati wa hedhi au hedhi yenye maumivu makali.
  • Hedhi ndefu au zinazorudia mara kwa mara.
  • Kuhisi Shinikizo au maumivu ya nyonga.
  • Kukojoa mara kwa mara au kupata shida wakati wa kukojoa.
  • Tumbo kuongezeka ukubwa.
  • Kukosa choo.
  • Maumivu ya tumbo, mgongo wa chini au maumivu wakati wa tendo la ndoa.

Fibroid inaweza kusababisha maumivu makali ikiwa inakosa mtiriiko wa damu na kuanza kupoteza mishipa mingi.

2.Aina kuu zauvimbe kwenye kizazi (uterine fibroids):

  • Intramural: Hukua ndani ya ukuta wa misuli ya uterasi.
  • Submucosal: Hujitokeza ndani ya tundu la uterasi.
  • Subserosal: Hujitokeza upande wa nje wa uterasi.

3.Lini ni Muda sahihi wa kumuona Dakitari.

Wasiliana na daktari kwa haraka sana ikiwa una:

  • Maumivu ya nyonga yasiyoisha.
  • Hedhi nzito au yenye maumivu yanayokuzuia kufanya shughuli zako.
  • Kutokwa damu kati kati ya kipindi cha mzunguko.
  • Unapata Shida ya kutoa mkojo.
  • Unapata Uchovu wa mara kwa mara (dalili za upungufu wa damu).

Pata matibabu ya haraka iwapo una hali ya kutokwa na damu nyingi sana ukeni au maumivu makali ya ghafla ya nyonga.

sababu za uvimbe kwenye kizazi.

Makala zaidi: Hali ya kutokwa na uchafu ukeni | Mambo 8 ya Kuzingatia

4.Sababu Uvimbe kwenye kizazi.

sababu za uvimbe kwenye kizazi ambazo ni za moja kwa moja-Hazijulikani , lakini kuna mambo yanayohusiana ni ukuaji wa vimbe hizi ni pamoja na:

  • Mabadiliko ya vinasaba (genes).
  • Mabadiliko makubwa ya Homoni (estrogen na progesterone).

Huchochea ukuaji wa fibroids na hufanya zikue wakati wa umri wa uzazi. Baada ya kukoma hedhi, fibroids huwa zinapungua.

  • Vichocheo vya ukuaji na extracellular matrix (ECM). Huchangia ukuaji na uimara wa fibroids kuendelea kuwepo na kukua zaidi.

5. Hali Hatarishi zaidi kwa uvimbe kwenye kizazi.

  • Umri wa uzazi.
  • Rangi: Watu weusi wana uwezekano mkubwa wa kuwa na fibroids, wakiwa wadogo zaidi, na mara nyingi wakipata fibroids huwa kubwa zaidi.
  • Historia ya kifamilia. Ikiwa mama au dada ana fibroids, hatari yako ya kupata fibroids huongezeka zaidi.
  • Mambo mengine: Kuanza hedhi mapema (kuvunja ungo kabla ya miaka 10), unene kupita kiasi, upungufu wa vitamini D, ulaji mwingi wa nyama nyekundu na ulaji kidogo wa mboga/ matunda/ ulaji mkubwa wa maziwa, na unywaji wa pombe.
madhara ya uvimbe kwenye kizazi

Makala zaidi: Mzunguko wa hedhi | Mambo 9 Muhimu Kuyafahamu.

6.Madhara ya Vimbe kwenye kizazi.

Fibroids mara nyingi hazina hatari nzito za moja kwa moja hasa kama hauna shida ya kuwa na watoto, lakini zinaweza kusababisha madhara fulani kwa mwingine anaweza asione kama ni mazito. haya ni Baadhi ya madhara ya uvimbe kwenye kizazi:

  • Maumivu makali mno ya nyonga.
  • Upungufu wa damu (anemia) mara kwa mara kutokana na kutokwa damu nyingi sana wakati wa hedhi, pia kusababisha uchovu mwingi.
  • Kukwamisha juhudi za kushika mimba.Mara nyingi sana vimbe kwenye kizazi ni kikwazo cha mimba kushika kutokana na mvurugiko wa homoni na mwingiliano wa mirija ya uzazi kuziba.
  • Katika ujauzito (ikiktokea umepata), zinaweza kuongeza hatari ya:
    • Placental abruption (kondo la nyuma kujitenga na uterasi(kuachia).Hali hii inaweza kupelekea kujifungua kwa upasuaji
    • Kukua kwa mtoto kwa shida (fetal growth restriction).
    • Kujifungua mapema kabla ya wakati (Mtoto njiti).

7.Jinsi ya Kuzuia uvimbe kwenye kizazi.

Japo Hakuna njia Moja ya moja kwa moja iliyokamili ya kuzuia fibroids, lakini unaweza kupunguza hatari kwa:

  • Kudumisha uzito mzuri.
  • Kufanya mazoezi mara kwa mara.
  • Kula lishe yenye matunda na mboga nyingi.
  • Kuepuka au kupunguza vyakula vyenye estrogen nyingi kama: vyakula vya kukaangwa, maziwa, mayai, nyama nyekundu n.k

Baadhi ya tafiti zinaonyesha dawa za kuweka sawa mpangilio wa homoni zinaweza kupunguza hatari, lakini utafiti zaidi unahitajika.

Je unasumbuliwa na Tatizo hili na ungependa kupata ushauri wa moja kwa moja kuhusu Mpango wa Tiba ya kuondoa uvimbe bila upasuaji? Tuma ujumbe wenye neno TIBA YA UVIMBE Kwenda WhatsApp 0711 556 377

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *