Vyakula bora kwa watu wenye kisukari
Superstar Foods”zinazosaidia kudhibiti sukari ya damu
Neno “superfood”hutumika sana kwenye mitandao na matangazo ya vyakula, lakini halina tafsiri rasmi ya kitabibu. Hata hivyo, kuna vyakula ambavyo vina mchango mkubwa sana katika kudhibiti kisukari na kulinda afya kwa ujumla.
Vyakula hivi vya mgonjwa wa kisukari vina:
Protini bora
Mafuta yenye afya
Vitamini na madini
Antioxidants
Nyuzinyuzi (fiber)
Kwa mtu mwenye kisukari, uchaguzi sahihi wa chakula ni dawa ya msingi.

Kanuni ya Sahani ya Kisukari
Katika mlo mmoja:

Nusu ya sahani: mboga zisizo na wanga mwingi
Robo ya sahani: protini
Robo ya sahani: wanga wenye ubora (complex carbohydrates)

  1. Mboga Zisizo na Wanga Mwingi
    (Non-starchy vegetables)
    Mboga hizi zinapaswa kujaza nusu ya sahani yako.
    Mboga za Majani ya Kijani Kiza
    (Spinachi, sukuma wiki,kale)
    Faida zake:
    Kalori chache
    Wanga kidogo
    Vitamini A, C, K, folate
    Madini kama chuma, kalsiamu, potassium
    Husaidia:
    Kudhibiti sukari ya damu
    Kulinda moyo
    Kuimarisha kinga

Parachichi (Avocado)
Parachichi ni chanzo kizuri cha:
Mafuta yenye afya (heart-healthy fats)
Nyuzinyuzi
Vitamini mumunyifu kwenye mafuta
Husaidia:
Kushiba kwa muda mrefu
Kudhibiti hamu ya kula
Kulinda afya ya moyo (muhimu sana kwa wagonjwa wa kisukari)

  1. Vyakula vya Protini bora
    Protini inapaswa kujaza robo ya sahani.
    Maharage, Kunde na Jamii ya Mikunde
    (Maharage, dengu, choroko, njegere, chickpeas)
    Faida:
    Protini ya mimea
    Nyuzinyuzi nyingi
    Folate, chuma, zinki, potassium
    Ingawa vina wanga, kiasi sahihi:
    Husaidia kudhibiti sukari
    Hakina mafuta mabaya kama nyama yenye mafuta mengi

Samaki Wenye Omega-3
(Salmon, sardine, mackerel, trout)
Omega-3:
Hulinda moyo
Hupunguza uvimbe (inflammation)
Hupunguza hatari ya magonjwa ya moyo
Ni vyema:
Kuchemsha, kuoka au kuchoma
Kula angalau mara 2 kwa wiki

Karanga na Mbegu
(Walnuts, karanga, flax seeds, chia)
Faida:
Mafuta yenye afya
Magnesium
Nyuzinyuzi
Husaidia:
Kudhibiti njaa
Kupunguza kula kupita kiasi
Baadhi zina omega-3 asilia

  1. Vyakula bora vya wanga (Carbohydrates)
    Wanga kwa mgonjwa wa kisukari hauondolewi kabisa, bali huchaguliwa kwa busara.
    Matunda Madogo (Berries)
    (Strawberry, blueberry, raspberry)
    Faida:
    Antioxidants
    Vitamin C & K
    Nyuzinyuzi
    Sukari ya asili isiyopandisha sukari haraka
    Ni mbadala mzuri wa vitu vitamu vyenye sukari nyingi.

Matunda ya jamii ya citrus
(Machungwa, ndimu, limau, grapefruit)
Faida:
Vitamin C
Nyuzinyuzi
Folate na potassium
Ni bora kula tunda zima, si juisi, ili kupata fiber.

Nafaka zisizokobolewa
(Oats, quinoa, mchele wa kahawia, shayiri)
Faida:
Nyuzinyuzi nyingi
Vitamini B
Magnesiamu na madini mengine
Hutoa nishati taratibu bila kupandisha sukari ghafla.
Maziwa ya mtindi:
Hutoa kalsiamu
Mara nyingi huongezewa Vitamin D
Kwa mgonjwa wa kisukari:
Chagua bidhaa zisizo na sukari iliyoongezwa
Epuka mtindi wenye ladha tamu
Mtindi wa kawaida pamoja na matunda kidogo ni chaguo bora

Jinsi ya kula vizuri bila gharama kubwa
Lishe ya kisukari si lazima huwa ni ghali:

Nunua vyakula vya msimu
Tumia mboga zilizogandishwa au za kopo bila sukari au chumvi
Osha mboga za kopo kupunguza chumvi
Tumia maharage makavu na nafaka unazopika mwenyewe
Nunua samaki wa bei nafuu waliogandishwa

Hitimisho muhimu
Kwa mtu mwenye kisukari:
Hakuna chakula cha miujiza
Mchanganyiko sahihi wa vyakula ndiyo ufunguo
Mboga nyingi, protini bora, wanga wa ubora, mafuta yenye afya
Lishe sahihi:
Hudhibiti sukari ya damu
Hulinda moyo
Hupunguza madhara ya muda mrefu ya kisukari