Ugonjwa wa PID ni Nini?

PID (Pelvic Inflammatory Disease) ni maambukizi katika viungo vya uzazi vya mwanamke, kama vile mji wa mimba (uterasi), mirija ya fallopia, na ovari. Ugonjwa huu mara nyingi husababishwa na maambukizi ya bakteria, hasa yale yanayotokana na magonjwa ya zinaa kama vile chlamydia na gonorrhea.

Katika kujibu hoja ya Msingi Kuhusu Pid ni Nini? Hapa kuna mambo 10 ambayo huenda hukuyajua kabisa kuhusu ugonjwa wa PID:

1. PID Inaweza Kutokea Bila Dalili Dhahiri.

Baadhi ya wanawake wenye PID hawaonyeshi dalili yoyote, hivyo ugonjwa huu unaweza kuendelea bila kutibiwa na kusababisha madhara makubwa.

Katika hali nyingi, wanawake hawa wanaweza kuishi na maambukizi haya bila kuwa na uelewa wa hali zao, na hivyo kuwa na hatari ya kupata matatizo makubwa zaidi. Matatizo kama vile mimba kuharibika mara kwa mara, mimba kutunga nje ya kizazi, Pamoja na mirija ya uzazi kuziba.

Ni muhimu kwa wanawake kufanya uchunguzi wa afya mara kwa mara ili kubaini hali yoyote isiyo ya kawaida, kwani matibabu ya mapema yanaweza kusaidia katika kuzuia matatizo makubwa kujitokeza hapo baadaye.

pid ni nini-hatua za kusambaa kwa maambukizi kwenye kizazi

Makala Zaidi:Zijue dalili za mimba changa | Dalili 12 za awali.

2. PID ni nini? – Husababishwa na Bakteria

PID hutokana na bakteria wanaoenea kutoka kwa uke hadi kwenye viungo vya ndani vya uzazi. Mara nyingi, husababishwa na maambukizi ya zinaa, lakini pia inaweza kutokea kutokana na bakteria wa kawaida wa uke kupenya ndani ya mwili.

3. Dalili Zake Zinaweza Kufanana na Magonjwa Mengine

PID inaweza kusababisha dalili kama maumivu ya tumbo la chini, kutokwa na uchafu usio wa kawaida ukeni, maumivu wakati wa tendo la ndoa, homa, au kuhisi uchovu mwingi. Dalili hizi zinaweza kufanana na magonjwa mengine kama UTI au endometriosis.

Mara nyingi, wanawake wanaweza kudhani kuwa wana matatizo mengine yanayohitaji matibabu tofauti, na hivyo wanakosa kupata huduma stahiki. Wanjikuta wanatibu kile wasichoumwa, halafu kile wanachoumwa  Hawakifanyi Matibabu. Ndipo Tatizo linaendelea kuwa kubwa zaidi.

pid ni nini ukilinganisha na mahonjwa mengine

Makala Zaidi: Tatizo la kutoona siku za hedhi | sababu na Matibabu yake.

4. PID Inaweza Kusababisha Ugumba

PID inapoathiri mirija ya fallopia, inaweza kusababisha kovu na kuziba mirija hiyo, jambo linaloweza kuzuia yai kufika kwenye mji wa mimba na kusababisha ugumba.

Kadiri ugonjwa unavyoendelea bila matibabu, ndivyo madhara yanavyoweza kuongezeka, na hivyo kusababisha tatizo linaloweza kuathiri sana uwezo wako wa kushika mimba.

Wakati mirija ya fallopia inapozibwa au kuharibiwa, kuna hatari kubwa zaidi ya mimba Kutunga nje ya kizazi, ambazo ni hali ya hatari zaidi kwa maisha ya mama.

pid ni nini, mwonekano wake kwenye kizazi

Makala Zaidi: P.I.D Ni nini? | Dalili, Sababu na Matibabu.

5. PID Inaongeza Hatari ya Mimba Kutunga Nje ya Mji wa Mimba

Kwa sababu PID inaweza kuharibu mirija ya fallopia, yai lililorutubishwa linaweza kujishikiza nje ya uterasi, hali inayojulikana kama mimba ya nje ya mji wa mimba, ambayo ni hatari kwa afya ya mama.

6. Kwa kawaida PID Inahitaji Matibabu ya Haraka.

Matibabu ya PID yanajumuisha matumizi ya Dawa zenye uwezo mkubwa wa kumaliza Tatizo, lakini ikiwa haitatibiwa kwa wakati, inaweza kuleta madhara ya kudumu kwa mfumo wako wa uzazi.

Unhitaji Matibabu ya haraka Pale Unapokuwa na Baadhi ya Dalili kama Vile kutokwa na uchafu ukeni, Maumivu ya tumbo chini ya kitovu,maumivu wakati wa tendo la ndoa, Miwasho ukeni, kutokwa uchafu kama Maziwa Mtindi.

7. Njia Kuu ya Kujikinga ni Kuepuka Maambukizi ya Zinaa.

Kwa kuwa magonjwa ya zinaa ni chanzo kikuu cha PID, matumizi sahihi ya kondomu na kuwa na uhusiano wa mpenzi mmoja mwaminifu husaidia kupunguza hatari ya kuambukizwa Ugonjwa huu.

ujue ugonjwa wa pid unavyosababisha madhara kama nini

Makala Zaidi: Maumivu ya tumbo la hedhi (Dysmenorrhoea | chango la uzazi

8. PID Inaweza Kujirudia

Kama umewahi kupata PID mara moja, kuna uwezekano mkubwa wa kuipata tena ikiwa hutachukua tahadhari za kutosha, Kujiepusha na Tatizo hilo. Hii huongeza hatari ya matatizo ya kiafya kama ugumba (Kupata shida ya kushika mimba).

Hakikisha unatibu Tatizo Linaisha kabisa Kisha Unapata Ulinzi Mathubuti ili Kuzuia Hali Hiyo Kujitokeza tena.

9. Vipimo vya Mapema ni Muhimu kwa Kinga ya PID.

Kwa wanawake walio katika hatari, kama wale walio na historia ya magonjwa ya zinaa, ni vyema kupima mara kwa mara ili kugundua na kutibu PID mapema.

10. PID Inaweza Kuepukika.

Njia bora ya kuzuia PID ni kutunza afya yako ya uzazi, kufuata Taratibu bora za usafi mzuri wa uke, na kuepuka tabia hatarishi kama ngono zembe au matumizi mabaya ya antiseptic zinazoweza kuharibu bakteria wazuri wa uke (Mfano: Hakikisha hauingizi ukeni Mapovu ya sabuni, wala manukato, wala marashi-Kwa sababu hayo yanaweza kubadilisha Ph ya Ukeni).

Lakini pia Kutokuwa na Mazoea ya Kujichokonoa ukeni (Kuosha mara kwa mara). Na Kuhakikisha unakojoa Mara baada ya tendo la ndoa na Kuosha sehemu za siri, na kuoga kila baada ya tendo la ndoa ni Muhimu katika kuzuia uzalianaji wa vimelea

Hitimisho:

PID ni ugonjwa hatari unaoweza kusababisha madhara makubwa kwa afya ya uzazi wa mwanamke. Kupata elimu, kutumia kinga, na kupima mara kwa mara kunaweza kusaidia kuzuia na kugundua tatizo hili mapema. Ikiwa una dalili zozote za PID, Pata Msaada wa Matibabu Yenye Kumaliza kbisa tatizo hili bila kujirudia. Bofya Hapa.